Tuesday, 11 November 2014

5 Personal Secretaries Wanted in TanzaniaBabati is recruiting 5 Personal Secretaries III

Deadline: 25 November 2014

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati, anawatangazia wananchi wote wenye sifa, nafasi za kazi kama ifuatavyo:-
KATIBU MUHSUSI DARALA LA III (PERSONAL SECRETARY III) TANO NGAZI YA MSHAHARA TGSB.

SIFA ZA MWOMBAlI:

Awe na Elimu ya Kidato cha nne au sita.
Awe amehitimu mafunzo ya Uhazili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na kufaulu mtihani hatua ya tatu.
Awe amepata mafunzo ya Komputa kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika Programu za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher


APPLICATION INSTRUCTIONS:

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA:
Mwombaji awe Raia wa Tanzania na awe tayari kufanya kazi sehemu yoyote kwenye Halmashauri ya Mji wa Babati.
Barua za maombi ziambatanishwe na nakala za vyeti vya elimu, Taaluma, Cheti cha kuzaliwa na picha mbili za rangi (Passport size)
Barua za maombi ziambatanishwe na maelezo Binafsi ya mwombaji (CV).
Waombaji waliosoma nje ya nchi, waambatanishe uthibitisho wa vyeti vyao kutoka Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni saa 9:30 Alasiri.
Waombaji wote wanatakiwa wawe na umri usiozidi miaka 45.
Maombi vote yatumwe kwa anwani ifuatayo:

Mkurugenzi wa Mji, Halmashauri ya Mji,
S. L. P. 383,
BABATI.