Monday, 2 September 2013

Fundi Ushonaji-Tailors at Lifa Enterprises Limited

Job Title; Fundi Ushonaji-Tailors

Employer: Lifa Enterprises Limited


Duty Station: Arusha

Application Deadline: 14th Sept 2013


Job Description:
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Kampuni ya LIFA ENTERPRISES LIMITED inakaribisha maombi ya kazi kwa watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi nne (4) kama ifuatavyo:
FUNDI USHONAJI (FUNDI CHEREHANI) (TAILORS)-NAFASI 4
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
•         Kushona nguo kulingana na mahitaji ya mteja.
•         Kushauri mteja kulingana na huduma anayohitaji.
•         Kutunza vitendea kazi ya ofisi.
•         Kusimamia kazi zote za mteja.
•         Kuweka kumbukumbu nzuri za wateja.
•         Kutathimini (monitoring )viwango vya kazi zinazohitajika kufanyika
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
•         Waliofuzu mafunzo ya cheti kutoka Chuo Cha Ufundi kinachotambuliwa na Serikali katika fani ya ushonaji (Sewing).
•         Kuajiriwa wenye vyeti (Cheti) cha mafunzo ya ushonaji (Tailoring) kutoka VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
•         Wawe na ujuzi wa kutumia aina zote za mashine za kushonea (Sewing Machine).
•         Wawe na uwezo wa kushona na kutarizi.
•         Wawe wabunifu wa mavazi na uwezo wa kushona nguo za aina zote.
1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Uwezo wa kazi na mishahara ya ofisi.

NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI YOTE.
1)      Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
2)      Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
3)      Maombi yote yaambatane na nakala ya vyeti vya taaluma, maelezo, kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo ya ushonaji kwa kuzingatia sifa za kazi. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka/kupotea.
4)      Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 14 Septemba, 2013
5)      Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo:-
MKURUGENZI MTENDAJI,
LIFA ENTERPRISES LIMITED,
P.O.BOX 14081.
ARUSHA-TANZANIA.