Monday, 12 August 2013

WAHAMASISHAJI UPANDAJI MITI-DAWA Jobs at Neema Herbalist Co. LTD in Tanzania

Job Title: WAHAMASISHAJI UPANDAJI MITI-DAWA.

Employer: Neema Herbalist Co. LTD

Duty Station: Dar Es Salaam

Application Deadline: 28th Aug 2013

Job Description:
 
Neema  HERBALIST & Co. LTD  ni   kampuni  inayo  jishughulisha  na  uhamasishaji  wa  matumizi  ya  dawa  asilia  nchini  Tanzania.  Tunatangaza  nafasi  za MAFUNZO    ya   KUHAMASISHA   UPANDAJI  MITI-DAWA . Wahitimu  wa  mafunzo   haya watapata  nafasi  ya  kufanya   kazi   ya  kuelimisha  wananchi  kuhusu  upandaji  wa  miti  dawa pamoja  na  kuhamasisha  watu kuhusu  matumizi  ya  dawa  asilia  katika  wilaya zote  za  Tanzania  bara .
SIFA   ZA   MWOMBAJI:
1.    Umri  miaka 18  hadi  45.
2.    Elimu  ya  kuanzia  kidato  cha  nne, sita  na kuendelea.
3.    Awe na  uwezo  wa  kuwasiliana  kwa  lugha  za  Kiswahili  na  kiingereza. 
4. Awe  mkaazi  wa  wilaya  ya  Kinondoni, Ilala  au  Temeke.
4.    Awe  tayari  kufanya  kazi  kwa  muda wa  mwaka  mmoja  kama    muelimishaji  kuhusu  upandaji wa  miti dawa pamoja  na kuhamasisha  watu  kuhusu umuhimu  wa  matumizi  ya  dawa  asilia  katika  wilaya  yoyote  ya   Tanzania  bara.
 
ADA  YA  MAFUNZO:Ada  ya  mafunzo  haya  ni  shilingi  Laki  Moja  na  Elfu  Ishirini  na  Tano  tu ( Tshs.125,000/=).
FOMU ZA MAOMBI   YA  KUJIUNGA  NA  MAFUNZO: Fomu  za   maombi  ya  kujiunga  na  mafunzo  haya zinapatikana  ofisini  kwetu  kwa  shilingi  Elfu  Kumi  na  Tano  tu! ( Tshs.15,000/=).
TAREHE  YA  KUANZA  KWA  MAFUNZO: Mafunzo  haya  yataanza   rasmi  siku  ya  tarehe   02 Septemba  2013   na  yatafanyika  kwa  muda  wa  wiki  tatu.
BAADA  YA  KUMALIZIKA  KWA  MAFUNZO:  Baada  ya  kumalizika  kwa  mafunzo  haya, wahitimu  wote  watapata  nafasi  ya  kufanya  kazi   katika  Mradi  wa  Kuhamasisha  Upandaji  Miti-Dawa  Tanzania, (   GROW  HERBS  CAMPAIGN )  kama  waelimishaji  na  wahamasishaji  kuhusu  upandaji  wa  miti  dawa  pamoja  na  matumizi  ya  dawa  asilia  katika  wilaya  mbalimbali  za  Tanzania  bara kuanzia  tarehe  01 OKTOBA  2013.

UTARATIBU  WA  KUPATA  FOMU: Fomu za  maombi  ya  kujiunga  na  mafunzo  haya, zinapatikana katika ofisi  zetu  zilizopo jijini  Dar  Es  salaam,  katika  eneo  la  CHANGANYIKENI karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU.
 
 
MWISHO   WA   KUPOKEA  MAOMBI NI  TAREHE   28 AGOSTI  2013

 
How to Apply:
Kwa  taarifa zaidi  kuhusu  mradi  huu, tembelea ; http://www.neemaherbalist.blogspot.com